UWEZESHAJI, UHIFADHI WA CHAKULA CHA MIFUGO

Changamoto kubwa inayowakabili wafugaji wanaotegemea malisho ya asili hasa kwa kipindi cha kiangazi ni ukosefu wa chakula cha mifugo. Tofauti na wakati wa masika ambapo mifugo inanona na kutoa maziwa mengi, wakati wa kiangazi mifugo hukonda na kuwa na uzalishaji mdogo wa maziwa au kukosa kabisa maziwa.