PASS Trust, Yajidhatiti Kuimarisha Mifumo Ya Chakula Nchini

Nchi nyingi Barani Afrika, changamoto ya upatikanaji wa chakula bado ni kubwa. Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimebarikiwa kuwa na ardhi yenye rutuba ambayo inaruhusu uzalishaji wa mazao mbalimbali, Hali hii imefanya taasisi nyingi zinazojihusisha na sekta ya kilimo kuwekeza zaidi katika sekta hii. Teknolojia za uzalishaji zimeboreshwa, zitoa fursa kwa wajasiriamali na uhakika wa upatikanaji wa chakula. Makala hii inanaangazia jinsi PASS Trust na teknolojia za kilimo zinavyoleta mabadiliko katika sekta ya kilimo na kusaidia kuinua ajenda ya upatikanaji wa chakula nchini.

Wafanyakazi wakiendelea na shughuli za uzalishaji katika kiwanda kimoja wapo kilichopata dhamana ya mkopo wa kilimo kupitia PASS Trust kutoka Kanda ya Kaskazini.

Mkurugenzi mtendaji wa PASS Trust Bw. Yohane Kaduma, Anasema kuwa, “uwepo wa teknolojia hizi za uzalishaji hasa katika sekta ya kilimo, umetatua changamoto nyingi sana kwa wakulima, kwakuwa sasa wanaweza kulima hekari nyingi za mashamba kwa kutumia trekta na zana mbalimbali za kilimo “. “Sisi PASS Trust, kupitia huduma zetu tunawezesha upatikanaji wa dhamana za mikopo ya kilimo kwa wajasiriamali waliopo katika mnyororo wa kilimo ambapo kupitia mkopo huo wa fedha wakulima wanaweza kununua zana za kisasa za uzalishaji kama vile trekta, taa za sola, mifumo ya umwagiliaji, pawatila, na mahitaji yote yanayohusisha teknolojia za kisasa katika uzalishaji”.

Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust, Yohane Kaduma akizungumza na wadau wa kilimo kwenye moja ya Mkutano uliyofanyika katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Anaeleza Kaduma hadi sasa, Kuna miradi zaidi ya 72,201 iliyodhaminiwa na PASS Trust katika mikoa mbalimbali hapa nchini, Ambapo wajasiriamali waliopo katika mnyororo wa thamani wa kilimo wameweza kunufaika na fedha hizo ambazo zimewasaidia kununua zana za kisasa za uzalishaji ambazo zinaleta uhakika wa upatikanaji wa chakula.

Ili kuhakikisha uzalishaji unakuwa endelevu na changamoto za upatikanji wa chakula zinafika kikomo, PASS Trust imedhamini mikopo yenye dhamani ya zaidi ya TZS 1.5 Trioni na kufanikiwa kutengeneza ajira takribani 2.7 kwa vijana na wanawake ambao ni sehemu ya wanaufaika wa mkopo huo. Kundi hili sasa wanauwezo wakununua zana za kisasa za uzalishaji kupitia mkopo wa fedha waliodhaminiwa na PASS Trust ili waweze kukuza uzalishaji wao.

Wakulima wakiwa kwenye picha ya pamoja katika zana za kilimo zipatazo 28 (trekta za mikono – power tillers) walizokabidhiwa kupitia dhamana ya mkopo wa kilimo kutoka PASS Trust kwa ushirikiano na Benki ya Equity pamoja na Kampuni ya Agricom kutoka Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Katika kundi hili la vijana na wanawake, jumla ya wanufaika milioni 3.5 wa PASS Trust, 45% ni wanawake na kati ya hawa 516,606 ni wanufaika wa dhamana ya kijani. Ambapo mjasiriamali anaezalisha kwa kuzingatia ukuaji wa uchumi wa kijani shirikishi anapata dhamana ya mkopo hadi 80%.

Mkurugenzi mtendaji wa PASS Trust Bw. Kaduma anasema kuwa “PASS Trust ina vijana 381 ambao wamehitimu katika vituo atamizi (Agribusiness Innovation Center – AIC) huko Kongwa jijini Dodoma na wengine wakiwa SUA mkaoni Morogoro. Vijana hawa wanaujuzi wa teknolojia ya kisasa ya uzalishaji wenye tija, Hivyo kupitia mafunzo waliyoyapata katika vituo hivyo yatawasaidia wao kutumia teknolojia ya kisasa katika kuzalisha ili jamii yetu iendelee kuwa na uhakika wa chakula”.

Mkurugenzi Mtendaji wa PASS Trust, Yohane Kaduma akizungumza na wadau wa kilimo kwenye moja ya Mkutano uliyofanyika katika Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF) uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Uwepo wa teknolojia za kisasa za uchakataji wa mazao, Zinaongeza thamani na kusaidia wakulima kuweza kufikia masoko bora zaidi. PASS Trust imesaidia kutoa mafunzo na dhamana za mikopo ya fedha kwa wakulima ili ili watumie teknolojia za kisasa za kuchakata mazao yao kabla ya kuyapeleka sokoni na kuyafanya yahitajike zaidi sokoni. PASS Trust kwa kuanzisha kampuni tanzu ya PASS Leasing imerahisisha upatikanaji wa zana mbalimbali za kilimo kama vile trekta na mashine za kuvunia.