Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Ametembelea Banda la PASS Trust

DODOMA: Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe ametembelea Banda la PASS Trust katika Maadhimisho na Maonesho ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nane Nane – 2024) yanayofanyika Kitaifa katika Viwanja vya Nane Nane jijini Dodoma kuanzia tarehe 1 – 8 Agosti, 2024.

Ameweza kujionea juhudi za PASS Trust katika uwezeshaji wananchi kiuchumi katika sekta ya mifugo na uvuvi. Ambapo, ameipongeza PASS Trust kwa juhudi mbalimbali inazofanya katika uwezeshaji wananchi hasa katika sekta ya mifugo na uvuvi, kwani imekuwa na mchango mkubwa katika uzalishaji wa ajira na uboreshaji wa maisha yua mtu mmoja mmoja na taifa kiujumla.

Katika mazungumzo kuhusu PASS Trust, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa PASS Trust, Adam Kamanda, amesema, “Mpaka sasa PASS Trust imefanikiwa kuwawezesha kiuchumi wananchi wapatao 2,669,213 katika hawa, wanufaika wanaume ni 1,925,884 (48.8%) na wanufaika wanawake ni 2,019,695 (51.2%) na kupelekea kuzalisha ajira zipatazo 2,791,130. Uwezeshaji huu umegusa maeneo mbalimbali ya kilimo, ufugaji, uvuvi, mazao ya misitu, na viwanda.”

Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, Piga simu bure: 0800 750 037 kuanzia Jumatatu – Ijumaa, Saa 2:00 asubuhi – Saa 11:00 jioni.