Mkuu wa Mkoa wa Singida Mh. Halima Dendego ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza Kanda ya Kati upande wa maandalizi ya Nane Nane – 2024, ametembelea Banda la PASS Trust linalopatikana katika Viwanja vya Nane Nane jijini Dodoma kuanzia tarehe 1 – 8 Agosti, 2024 na kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika sekta ya kilimo, ufugaji, uvuvi, mazao ya misitu, na viwanda.
Katika mazungumzo yake na viongozi wa PASS Trust, Mh. Dendego ameipongeza PASS kwa juhudi zake za kuwawezesha wajasiriamali wa kilimo biashara wa mkoa wa Singida, ambapo, PASS Trust imekuwa na mchango mkubwa katika kuinua wakulima wanaolima mazao ya bishara na chakula.
Afisa wa PASS Trust, Henry Mchau ameelezea namna PASS Trust inavyotoa huduma za maendeleo ya biashara na huduma za fedha kwa wakulima, wafugaji, pamoja na wavuvi. Ambapo, imeweza kuwezesha vikundi na AMCOS vimefanikiwa kupata jumla ya mikopo ya Bilioni 275.8 kupitia dhamana za PASS Trust.
Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, Piga simu bure: 0800 750 037 kuanzia Jumatatu – Ijumaa, Saa 2:00 asubuhi – Saa 11:00 jioni.